Venue: Jimbo la Kilifi, Pwani
Theme: Kilifi Tuungane
Mnamo tarehe 10/10/2026 sote tuliandamana mpaka Jimbo la Kilifi, Pwani kuiweka historia katika daftari ya kumbukumbu. Kwa pamoja wanachama, wakazi, wakuu wa chama chetu na wale kutoka vyama vya United Alternative Government walikuja kushuhudia Uzinduzi Rasmi wa Ofisi Mpya ya Jimbo La Kilifi ikiwa lengo kuu ni kuleta huduma za chama karibu na wananchi, mathalani tunapojiandaa katika Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Hafla hii iliwaleta kwa pamoja wagombea viti mbalimbali kutoka kata mbalimbali, Pwani. Chama hiki cha Democratic Party of Kenya, kinazidi kuwa na ushawishi mkubwa haswa miongoni mwa wagombea vijana na wale wa jinsia ya kike; chama kinautambua umuhimu na mchango wao katika uendelezaji wa demokrasia, ubunifu na maendeleo.
Uzinduzi wa ofisi hii ya DP humu Kilifi ni ishara tosha kwamba chama cha DP kinawadhamini wakazi na wafuasi wake katika kanda la pwani. Hapo awali wagombea wa viti tofauti tofauti huko Kilifi walipata changamoto kuzipata huduma za chama, lakini hilo sasa limepita.
Kujiunga kama mgombea wa kiti cha MCA/MP/Women Rep/Senator/Governor wasiliana nasi kupitia 0798740778.


























